Klabu ya Soka ya Ruvu Shooting imeamua kuachana na kocha wake mkuu Mkenya Tom Alex Timamu Olaba na badala yake kumtumia Seleman Mtungwe ambaye imemsomesha hadi Daraja B.

Olaba alijiunga na timu ya Ruvu Shooting msimu wa mwaka 2014 mzunguko wa pili baada ya aliyekuwa kocha mkuu Boniface Mkwasa kuvunja mkataba na kuamua kwenda kuifundisha timu ya Young Africans ya Dar es salaam.

Wakati Olaba anaanza kuifundisha Ruvu Shooting msimu huo wa mwaka 2014/15 aliikuta ikiwa na point 17, mpaka mwisho wa ligi Ruvu Shooting chini ya Olaba ilimaliza ikiwa nafasi ya 5, point 35.

Msimu wa 2015/16 Ruvu Shooting chini ya mwalimu Olaba haikufanya vizuri kwani ilishuka Daraja ikiwa na jumla ya pointi.

Olaba pamoja na kushuka kwa Ruvu Shooting, alikubali kushuka nayo hadi ligi Daraja la Kwanza akiahidi kuipandisha daraja, ahadi ambayo aliitekeleza.

Katika ligi hiyo ya FDL maafande hao walicheza kwa mafanikio makubwa wakiwa kwenye kundi B lenye timu nyingine saba ambazo ni Polisi Morogoro, Lipuli (Iringa), Kurugenzi (Iringa), Mji Njombe (Njombe), Mlale JKT (Songea), Kimondo (Mbeya) na Burkinafaso (Morogoro).

Waulimaliza ligi hiyo tukiwa na jumla ya pointi 33 zilizotokana na ushindi wa michezo 10 kati ya 14, wakipoteza mchezo mmoja dhidi ya Mlale JKT (1-0) na sare tatu, dhidi ya Njombe Mji (2-2), Kimondo (1-1) na Polisi Morogoro (0-0). Hayo yalikuwa mafanikio makubwa sana kwa timu ya Ruvu Shooting na kocha Olaba.

Tom Alex Timamu Olaba

Kufuatia maamuzi ayoa mbayo bado hayajetolewa ufafanuzi wa kina, Uongozi wa Ruvu Shooting chini ya Mwenyekiti wake Kanali Charles Mbuge umemtakia kila la kheri Tom Alex Timamu Olaba, ambaye kwao ni kocha makini, Mahili, mcheshi, kutokana na uweledi na akili nyingi katika kufundisha soka.

“Ruvu Shooting tunaheshimu sana mchango wa Olaba katika timu yetu na tunamheshimu sana Olaba, tutaendelea kumheshimu na kuamini kuwa ni miongoni mwa makocha bora katika ukanda huu wa nchi za maziwa makuu na Afrika!”

“Ruvu Shooting tunamkumbuka, tutaendelea kummbuka kwa mema na mafanikio makubwa ndani ya timu yetu chini ya uongozi wake!”

“Mungu azidi kumbariki, kumpa afya, maisha marefu na mafanikio makubwa katika kazi yake ya kufundisha soka!” ilieleza taarifa iliyotolewa na afisa habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire.

Juventus Kumsajili Marko Pjaca
Mashoga 150 wapanga kummaliza Makonda, aanza kuwashughulikia