Ligi daraja la kwanza Tanzania Bara inaelekea ukingoni. Ligi hiyo itakayotoa washindani watatu wapya katika ligi kuu msimu wa 2016/17, imegawanywa katika makundi matatu na kila mshindi wa kundi atapanda moja kwa moja VPL msimu ujao.

KUNDI A:

Ni wazi ‘Wanajeshi’ wa Ruvu Shooting wamerejea tena VPL baada ya kushuka msimu uliopita.

Ikiwa na wastani wa magoli 18 zaidi ya Njombe Mji ya Njombe, Shooting imekusanya pointi 28 huku kila timu ikiwa imesalia na michezo mitatu.

Njombe inafuatia ikiwa na alama 19 na kwa mbali JKT Mlale ya Ruvuma, Kurugenzi FC ya Mafinga, Iringa zinafuatia zikiwa na alama 17 kila timu.

Polisi Moro FC imeachwa pointi 14 na Shooting ipo nafasi ya 5 ikiwa na pointi 14.

Kimondo FC ya Mbeya inekusanya alama 11 na timu hiyo itakuwa na vita ya kutoshuka dhidi ya Lipuli FC ya Iringa yenye alama 10 na waburuza mkia wa kundi A timu ya Burkina Faso FC ya Morogoro yenye alama 6.

Serikali yalitega shirika la Nyumba Nchini kuhusu 'Wabangaizaji'
Kama Itakua Hivi, Suleimani Matola Atakua Na Bahati Ya Kipekee