Serikali imewaagiza wakurugenzi nchini hasa kwenye maeneo wanayojishughulisha na uvuvi kuwachukulia hatua maafisa uvuvi wanaoshindwa kutimiza wajibu kwa kushindwa kuzuia uvuvi haramu.

Akizungumza baada ya kikao cha kamati kilichohusisha Wizara saba za Maliasili, Ulinzi, Nishati na Madini Tamisemi, Kilimo, Mifugo na Uvivi pamoja na Mambo ya Ndani Naibu Waziri TAMISEMI Suleiman Jaffo amewataka watendaji hao kutumia agenda ya kupambana na uvuvi haramu kuwa agenda ya kudumu  katika vikao vyao.

Amesema kuwa maafisa uvuvi hao wanatakiwa kupimwa wajibu na utendaji kazi kwa kuangalia ni kiasi gani wanajihusisha na masuala mazima ya kupambana na uvuvi wa kutumia mabomu.

“Kuna baadhi ya mafisa uvuvi wanahusika na vitendo vya uvuvi haramu nchini hivyo kuanzia kesho wataanza kupimwa wajibu wao na kwa atakayeshindwa kutimiza wajibu atatolewa katika nyazifa hiyo,”amesema Jaffo.

Kwa upande wake Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Januari Makamba, amesema kuwa nchi yetu inaeneo kubwa la bahari na kwa miaka kadhaa nchi yetu imekuwa na changamoto ya uvuvi haramu, hivyo tumeona kuna haja ya kuchukua hatua ya haraka katika kupambana na uharamia huo.

 

Nana Akufo- Addo aapishwa kuwa rais mpya wa Ghana
Samia suluhu atoa agizo kwa majaji nchini