Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Magufuli ametunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi 128 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). walio hitimu mafunzo yaliyoanza Januari 28, 2019 huku wengine 26 wakishindwa kutunukiwa kwa kutohitimu mafunzo hayo.

Hafla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa hao wapya  kwa cheo cha Luteni Ussu imefanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.

Akitoa taarifa kuhusu mafunzo hayo, mkuu wa chuo cha mafunzo ya maofisa wanafunzi wa Jeshi Monduli (TMA), Brigedia Jenerali Ibrahim Muhana amesema kati 126 waliohitimu chuoni hapo 101 ni wanaume na 25 ni wanawake.

Maafisa 28 ambao nao wametunukiwa Kamisheni wamehitimu katika vyuo vya Kijeshi vilivyopo kwenye nchi za China, Uingereza, India, Ujerumani, Kenya na Morocco.

Wakati wa hafla hiyo Maafisa 6 waliofanya vizuri wakati wa mafunzo walipewa zawadi

Tanzania yaongoza miradi mikubwa ya ujenzi EAC
Kobe na Gianna kuagwa rasmi