Maafisa watano wanaotoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa kupooza, polio, wamepigwa risasi na kuuliwa mashariki mwa Afghanistan.

Maafisa hao wameuawa leo kwa kushambuliwa katika maeneo matatu tofauti ndani ya saa chache kwenye mashambulizi ya kupangwa.

Msemaji wa jeshi la polisi mkoa wa Nangarhar, Farid Khan, amesema hiyo ni kazi ya kundi la Taliban kuwashambulia maafisa wa afya ili kuwanyima watu chanjo dhidi ya ugonjwa wa kupooza ingawa kundi la Taliban lenyewe limekanusha kuhusika na mashambulizi hayo.

Msemaji wa Wizara ya Afya ya Afghanistan, Osman Taheri, amethibitisha kutokea mashambulizi hayo.

Naye Afisa wa cheo cha juu wa Umoja wa Mataifa, Ramiz Alakbarov, ameyalaani vikali mashamblizi hayo.

Ugonjwa wa kupooza umetokomezwa kote ulimwenguni isipokuwa Afghanistan na Pakistan, ambako watu hawana imani na chanjo na wana wasiwasi kuhusu kampeni za kuutokomeza.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Juni 16, 2021
Mashindano ya Miss East Afrika kufanyika Novemba