Maafisa wa wawili wa Serikali ya Korea Kaskazini wanadaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi hadharani na silaha za kutungulia ndege (anti-aircraft gun), kwa makosa mawili tofauti ikiwa ni pamoja na kusinzia katika kikao kilichoendeshwa na Mkuu wa nchi hiyo, Kim Jong-Un.

Gazeti la Korea Kusini la ‘JoongAng Ilbo’ limeripoti kuwa Ri Yong-Jin ambaye alikuwa afisa mwandamizi katika idara ya elimu nchini humo, aliuawa kwa kosa la kusinzia katika kikao cha Kim Jong –U, lakini pia alikutwa na hatia ya makosa mengine ya rushwa baada ya kuhojiwa.

“Alikamatwa kwenye kikao hicho na kuhojiwa na wizara ya usalama na ulinzi. Aliuawa baada ya makosa mengine kubainika kama vile rushwa,” gazeti hilo limekinukuu chanzo chake.

Aidha, Hwang Min ambaye alikuwa Waziri wa Kilimo wa nchi hiyo aliuawa hadharani pia baada ya kuonekana kuwa aliwasilisha maoni ya mabadiliko ya sera ambayo yalionekana kama ni kuukosoa moja kwa moja utawala wa Kim Jong-Un.

Silaha za kutungulia ndege (anti-aircraft gun)

Silaha za kutungulia ndege (anti-aircraft gun)

Imeelezwa kuwa wawili hao waliouawa hadharani mwanzoni mwa mwezi huu kwa amri maalum kutoka kwa Kim Jong – Un katika eneo la kijeshi la Pyongyang.

Hata hivyo, Korea Kaskazini haijazungumzia taarifa hizo. Kwa mara kadhaa, taarifa kama hizi hukanushwa baadae na serikali hiyo na kuonekana sio za kweli.

CECAFA Kuanza Kushindanisha Timu Za Wanawake
Adrien Silva Athibitisha Kuihama Sporting Lisbon