Korosho ni moja ya nafaka muhimu sana katika mwili wa binadamu ijapokuwa hutumika kwa nadra sana kutokana na upatikanaji wake na gharama zake, Kwa Tanzania zao hili hulimwa kwa wingi katika mikoa ya pwani hasa Mtwara na Lindi ambapo katika msimu wa Korosho kilo moja ya Korosho hupatikana kwa gharama ya Shilingi Elfu thelathini kwa pesa ya kitanzania.

Kisayansi inashauriwa kutumia korosho kiasi, nafaka hii ina virutubisho muhimu na adimu, ambapo tafiti zilizofanyika zimebainisha kuwa mtu anayetumia korosho hufaidika kwa kuongeza vitu vifuatavyo mwilini.

Ina miliki calories 155, ni vyakula vivyohitajika mwilini ili kutengeneza nguvu na kuupa mwili virutubisho vyote vinavyotakiwa katika kujenga mwili, Ina miliki gram 9.2 za kabohaidreti, Gram 5.2 za Protini na Vitamini E, B6 pamoja na Gram 9.5 za vitamini K, Gram 10 za madimu ya ”Calcium” mbali na madini hayo ina umiliki mkubwa wa madini ya Zinki, Magneziam, Potasiam, kopa, na Asidi ya Folik.

Hivyo katika mwili wa binadamu korosho husaidia mambo yafuatayo

  1. Inasaidia kunyonya mafuta katika mwili wa binadamu hivyo huulinda mwili dhidi ya magonjwa ya moyo na kuusaidia moyo kuwa wenye afya njema.
  2. Huepesha ugonjwa wa Anemia na magonjwa mengine ya damu, kula korosho mara kwa mara husaidia mwili kuwa na madini ya chuma ambapo ugonjwa wa Anemia hutokana na upungufu wa madini ya chuma hivyo ulaji wa Korosho hukinga mwili na magonjwa ya damu ikiwemo Anemia.
  3. Korosho husaidia uwezo wa macho kuona kama ilivyo kwa karoti, kutokana na uchafuzi mkubwa wa mazingira macho yapo katika hatari kubwa ya kudhurika, korosho ina miliki kirutubisho kisayansi kinajulikana kama Zea Xanthin ambacho huilinda Retina ya jicho dhidi ya miale na uchafu ambao unaweza kudhuru jicho.
  4. Nzuri kwa kutunza ngozi, kutokana na mafuta yanayotokana na Korosho yenye virutubisho na madini rafiki kwa kung’arisha ngozi madini hayo ni kama Zinki, Magnesium, Fosforas na chuma lakini pia uwepo wa madini ya selenium ambayo hulinda ngozi dhidi ya magonjwa ya kansa.
  5. Lakini pia kwa wale wenye uhitaji wa kupunguza uzito, kisayansi inashauriwa kutumia kiasi nafaka ya korosho ili kupunguza uzito wa mwili, korosho inamiliki aina tatu za asidi ambazo husaidia mfumo unaoratibu mwili kuvunja vunja mafuta ya ziada.
  6. Pia mtu anayekula korosho ana wakati mzuri wa kufanya nyweli zake ziwe na afya nzuri hii ni kutokana na mafuta yanayotokana na korosho.

Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Croatia
Manuel Neuer kucheza tena wiki hii