Wanamitindo maarufu duniani kutoka nchini Argentina, Nadinne na Dannita wataka kuolewa na mwanaume mmoja hii ni kutokana na upendo walionao warembo hao licha ya kufanana wametaka pia kuolewa sehemu moja.

Wanamitindo hao ambao wamejipatia umaarufu nchini Argentina na duniani kote  kupitia maonesho ya kimataifa ya mitindo, wamesema kuwa hawawezi kuishi mbali wameshazoeana toka utotoni na hata kuolewa wataolewa na mwanaume mmoja.

Aidha mapacha hao ambao tayari wamefikisha umri wa miaka 30, wamesema kama Kanisa Katoliki nchini humo halitaruhusu ndoa ya mwanaume mmoja kuoa  wanawake wawili basi hawataolewa mpaka kufa kwao.

Mapacha hao ni moja ya warembo nchini Argentina wanaoingiza pesa ndefu zaidi mpaka sasa, wanatumia akaunti moja katika mitandao ya kijamii, na wameanzisha kampuni ya mavazi  ya watu 10 huku kampuni hiyo ikiingiza pesa nyingi kupitia post wanazoweka mitandaoni

Aidha Warembo hao wanalipwa kiasi cha dola $25,000 sawa na Tsh milioni 57 kwa wiki, hii ni kutokana na kuposti picha zao wakiwa kwenye maeneo ya Hotelini au Sehemu za kitalii kama Ibiza n.k .

Hata hivyo, warembo hao walishawahi kujitokeza na kukiri kuwa maombo yao sio ya asili wamefanyiwa upasuaji kuongeza makalio.

Masoud Djuma aikana Young Africans
Kikwete apongeza benki ya NMB

Comments

comments