Matunda yana faida nyingi sana za kiafya mwilini, Ukiachana na ladha tamu inayotokana na kula matunda, kila mtu anashauriwa ale matunda tofauti yasiyopungua matano (5) kwa siku ili kupata faida zote mwilini.

Faida kuu za matunda ni kuzuia maradhi, kurutubisha kinga ya mwili, kupunguza sukari kwenye damu, kungarisha ngozi, kuleta nguvu na kuleta mafuta asilia kwenye mwili.

Tunda la Fenesi ni moja ya tunda lenye virutubisho vingi kiafya ndani ya fenesi kuna virutubisho kama vile vitamin A, C na B6 pamoja na madini ya potassium na calcium sambamba na madini ya chuma na magnesium.

Tunda hili ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi yaani ‘fiber’ ambazo ni muhimu kwa upande wa umeng’enyaji wa chakula na hivyo kumsaidia mhusika kuepukana na shida ya kukosa choo mara kwa mara.

Lakini pia tunda hili huongeza vitamin C mwilini ambayo husaidia seli za damu kufanya kazi vizuri, lakini pia kama utakuwa na ngozi ambayo si nzuri labda huenda itakuwa na mikunjo mikunjo basi ni vyema ukaanza kutumia fenesi leo kwani litakusaidia kuondosha hali ya mikunjo kwenye ngozi na kuondosha ukavu wa ngozi.

Aidha, tunda hili la fenesi pia husaidia sana kwa wale wenye tatizo la presha ya kushuka hii ni kwa sababu ndani ya tunda hili kuna madini ya potassium ambayo hurekebisha kiwango sodium mwilini jambo ambalo huchangia kuongeza kwa kiwango cha msukumo wa damu mwilini.

Kampeni za Uchaguzi mkuu zasitishwa - Uganda
Ujerumani kuanza kutoa chanjo ya Corona