Mti wa mbuyu ni miongoni mwa miti yenye faida nyingi na maajabu mengi, vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu.

Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine yoyote unayoyajuwa. 

Zifuatazo ni faida za unga na juisi ya ubuyu kiafya:-

Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.

Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kashiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng’ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi!

Husaidia kujenga neva za fahamu mwilinilakini pia ia virutubisho vya kulinda mwili

Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambayo ni muhimu katika kuondoa sumu mwilini na umeng’enyaji wa madini ya chuma, kimsingi vyakula vyenye afya zaidi kwa ajili ya mwili ya binadamu huwa pia huwa na vitamin B2.

Inaongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C na pia ubuyu huongeza nuru ya macho na kwa wenye matatizo ya tumbo husaidia kuzuia kuharisha na kutapika

Ina magnesiam ambayo husaidia kujenga mifupa na meno

Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo

Unywe kiasi gani? Jipatie kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku hasa usiku na baada ya wiki kadhaa utaona matokeo yake mwilini.

Ili upate faida za juisi ya ubuyu, zinazoelezwa hapa, lazima upate ule ubuyu halisi (mweupe) usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha au rangi.

Fursa za uwekezaji Tanzania zaendelea kukua
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 23, 2021