Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa uongozi halali wa chama hicho haukubaliani na maamuzi yaliyofanywa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ya kukubali taaarifa ya Prof. Lipumba ya kuwafukuza wabunge wanane wa chama hicho.

Ameseyasema hayo visiwani Zanzibar alipokutana na Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho, ambapo amesema kuwa uamuzi huo wa Spika ni hujuma za kisiasa, hivyo ameitaka Jumuiya ya Umoja wa Mataifa kuingilia kati suala hilo.

Aidha, Maalim Seif ameitaka Jumuiya ya Umoja wa Mataifa kuingilia kati ikiwemo na kuiwekea vikwazo vya kiuchumi Tanzania pamoja visiwa za Zanzibar kwakuwa vitendo vya ukiukwaji wa sheria na Katiba vinazidi kushamili.

“Tunataka Jumuiya ya Kimataifa kuibana Tanzania kwa kuiwekea vikwazo vya kiuchumi na kuitenga kisiasa na Kidiplomasia hadi hapo watawala watakapoamua kuheshimu Sheria, Katiba, misingi ya Demokrasia, haki za binadamu na utawala bora,”amesema Maalim Seif.

Hata hivyo, Maalim Seif amesema kuwa kjufuatia kukubali taarifa ya Prof. Lipumba na kuchukua maamuzi ya haraka haraka, Spika wa Bunge amepoteza sifa na haiba ya kuongoza Bunge kwani Baraza Kuu la Chama hicho bado linawatambua wabunge hao waliofukuzwa uanachama na Prof. Lipumba.

 

Wakili wa Lissu amburuza kortini askari Polisi
Video: Yanga wammulika Niyonzima, Watakachoifanya Simba msimu ujao