Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amemuwekea mtego wa kisiasa mshindani wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa tiketi ya CCM, Dkt. Ali Mohamed Shein.

Akiwahutubia katika mkutano wa kampeni Chake Chake, Pemba, Maalim Seif amemtaka mpinzani wake huyo kuyarudia maneno aliyoyasema kwenye mkutano huo kuwa endapo mkutano utakuwa huru na haki atampongeza aliyeshinda.

“Jumapili tunakwenda kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu. Napenda kutamka bayana kwamba nikishindwa katika uchaguzi huru na haki nitampongeza aliyeshinda, lakini pia namtaka mwenzangu na yeye atamke hadharani kama mimi,” alisema.

Katika hatua nyingine, Maalim Seif aliwaahidi wananchi wa Zanzibar kuwa wakimchagua kuwa rais atafanya mabadiliko makubwa ikiwa ni pamoja na kusaidia kupatikana kwa muundo wa serikali tatu ili Zanzibar iwe dola kamili.

Maalim Seif pia alisema kuwa atapandisha kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma kuwa shilingi 400,000 na askari wa SMZ itakuwa shilingi 450,000.

Eminike Amfuata Enyeama Kwa Maamuzi Binafsi
Mbowe Aweka wazi Mpango Wa Ukawa Baada Ya Matokeo Kutangazwa