Katibu Mkuu wa Chama Cha wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amedai kuwa anaona dalili za Serikali kumkamata na kumfungulia mashtaka kutokana na harakati zake za kuendelea kuipinga Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akizungumza jana katika Msikiti wa Biziredi visiwani humo wakati wa ibada ya Ijumaa, Maalim Seif alidai kuwa anaona dalili za kukamatwa na kushtakiwa Mkoani Dar es Salaam, jambo alilodai ni mpango wa kufifisha juhudi zake visiwani humo.

”Kuna dalili za kutaka kunikamata wanipeleke Da es Salaam kama walivyofanya kwa masheikh, lakini nasema yote hayo ni kupoteza muda wa kuchelewesha haki ya Wazanzibari,” Maalim Seif amekaririwa.  ”Ieleweke kuwa haki hiyo haiwezi kuzuilika tena kwa sasa,” aliongeza.

Maalim Seif ambaye amekuwa akidai alishinda katika uchaguzi huo wa Oktoba 25 mwaka jana na kupokonywa ushindi wake na chama chake ambacho baadae kiliususia uchaguzi wa marudio. Amekuwa akizunguka ughaibuni na tayari amefikisha malalamiko yao kwenye Jumuiya ya Kimataifa.

Katika hatua nyingine, mwanasiasa huyo mkongwe na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mstaafu, alizungumzia madai ya Baraza la Mawaziri la Mapinduzi ya Zanzibar kutaka kujadili kuondolewa kwa mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) visiwani humo. Alisema kuwa hakuna anayeweza kufuta SUK kwani ilianzishwa kwa mujibu wa sheria  baada ya wananchi kupiga kura za maoni na maridhiano ya kisiasa.

Video: Taifa letu limepoteza ubunifu - RC Makonda
Mkurugenzi adai Lema amemdhalilisha, Gambo atoa msimamo