Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad ametangaza nia ya kugombea Zanzibar, amesema atachukua fomu Julai 4.

Amewaomba wazanzibari kumkubali kama walivyofanya kwa chaguzi zilizopita kwa kuongeza idadi ya wanaompigia kura kila uchaguzi mpya tangu mwaka 1995.

Amesema walifanya tafiti kuona kama wazanzibari bado wanamkubali na tafiti hiyo ilionesha kuwa bado anakubalika ndani ya Zanzibar.

Ameeleza tafiti waliyofanya ilionesha kuwa, kuna wazanzibar waliahidi kutopiga kura kama asipopewa turufu ya chama kugombea urais Zanzibar.

DAS Kisarawe atenguliwa kwa kashfa ya kuchukua wake za watu
JPM aipongeza DAWASA kujenga miradi kwa fedha za ndani