Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad jana aliruhusiwa kutoka katika hospitali ya Hindul Mandal iliyoko jijini Dar es Salaam baada ya kulazwa juzi kwa kile kilichoelezwa na madaktari kuwa kilitokana na uchovu wa safari ndefu ya ndege kutoka India alikoenda kupata matibabu.

Baada ya kutoka hospitalini hapo, Maalim Seif aliwahakikishia watanzania kuwa afya yake iko imara na kwamba anaweza hata kukimbia mbio za umbali mrefu.

“Kama mnavyoniona niko ‘fit’, nimelala usingizi mzuri leo na hali yangu imerudi kama kawaida, naweza hata kufanya mashindano ya kukimbia,” Maalim Seif anakaririwa.

Maalim Seif 2

Kiongozi huyo aliwashukuru Watanzania waishio ndani na nje ya nchi kwa upendo waliouonesha kwake kwa kutaka kufahamu hali yake kiafya wakati wote alipokuwa hospitalini hapo na mapokezi makubwa aliyoyapata katika uwanja wa ndege wa Amani Abeid Karume visiwani Zanzibar, alipotoka nchini India.

Maalim alieleza chanzo cha kulazwa katika hospitali hiyo, kinachokinzana na habari zilizokuwa zimeenezwa mitandaoni.

“Nilitoka nyumbani jana (juzi) nikiwa mzima wa afya, baada ya kuugua ghafla uwanja wa ndege, niliamua kuendelea na safari kwa kusaidiwa na wasaidizi wangu. Tuliamua kuja Hindu Mandal kwa ajili ya vipimo na matibabu,” alisema.

Mwanasiasa huyo alisisitiza kuwa Msimamo wa chama chake kutoshiriki uchaguzi wa marudio uko pale pale.

 

 

Real Madrid Watangulia Robo Fainali
Mkurugenzi Wa Ufundi ZFA Atumbuliwa Jipu