Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, atakuwa mikononi mwa Jeshi la Polisi visiwani Zanzibar Ijumaa hii akihojiwa.

Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdani Makame amethibitisha kuwa Jeshi hilo litamhoji Maalim Seif siku hiyo, japo hakubainisha chanzo cha mahojiano hayo pamoja na kile kitakachozungumzwa.

Kadhalika, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Salum Msangi aliwaambia waandishi wa habari kuwa Jeshi hilo litamhoji Maalim Seif kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea lakini hakueleza moja kwa moja na masuala gani.

Maalim Seif ameendelea kufanya mikutano ya hadhara, amewahamasisha wananchi kushirikiana na chama hicho kuikataa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwani wanaamini wao ndio walioshinda katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana.

Aliwapa mbinu wananchi wa Zanzibar kuwa wanaweza kuonesha ulimwengu kuwa hawaitaki Serikali hiyo kwa vitendo bila kufanya vurugu.

“Mfano, tunaweza kuamua siku fulani kuanzia saa sita, tunsimamisha vyombo vyote vya usafiri na siku nyingine tunaamua kupiga honi Zanzibar nzima kuonesha hatuitaki Serikali ya CCM,” alisema Maalim Seif katika moja ya mikutano yake hivi karibuni.

Mourinho Afungasha Kila Kilicho Chake Jijini London
Ali Kiba azivimbia tuzo, asema ni biashara tu