Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amewataka wananchi wa visiwa hivyo wasikubali kuchokozwa.

Maalim Seif aliyasema hayo katika kikao alichofanya na wajumbe wa kamati za utendaji za wilaya na majimbo visiwani humo. Siku moja baada ya kufanya kikao cha faragha na Dkt. Ali Shein aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM.

Aliwataka kuwa watulivu na kutokubali kufanya fujo  kuchokozwa na kufanya vurugu kutokana na hali iliyopo visiwani humo baada ya Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha kutangaza kufuta uchaguzi uliofanyika visiwani humo.

Alidai kuwa kuna watu wanaweza kuanza kufanya vitimbi kwa lengo la kutaka kuvuruga amani iliyopo visiwani humo.

Katika hatua nyingine, Maalim Seif aliwaeleza wanachama hao kuwa wasiwe na wasiwasi bali wasubiri aapishwe kuwa rais na wajionee maendeleo, huku akiwashukuru kwa ushiriki wao katika kupiga kura.

“Tamko la Mwenyekiti wa ZEC halina mashiko kisheria, ni lake binafisi,” alisema Maalim Seif. “Ngojeni Rais wenu atangazwe, aapishwe muone maendeleo ya nchi,” aliongeza.

Nazo nchi za magharibi ikiwemo Marekani na Uingereza zimeeleza kuridhishwa na hatua za mazungumzo zinazoendelea visiwani Zanzibar kati ya wagombea urais wa CCM na CUF kwa lengo la kutatua mgogoro huo wa uchaguzi.

 

Shilole Akiri Kufuatwa Na Wauza 'Unga'
Mabalaa Yaendelea Kuishukia Chelsea