Zaidi ya watu milioni 9.3 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona ulimwenguni kote huku Watu zaidi ya 481,000 wakiwa wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.

Ambapo wataalam wa afya nchini Marekani wametahadharisha kwamba hospitali za nchini humo zinaweza kukabiliwa na wingi wa wagonjwa wa COVID 19 kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona katika siku za hivi karibuni nchini.

Hata hivyo Majimbo yaliyokumbwa zaidi na ongezeko la maambukizi ya Corona ni Florida na Texas

Wakati huo huo Brazil imethibitisha na maambukizi mapya 40,700 huku idadi mpya ya vifo ikiwa ni zaidi ya watu 1,100.

CHADEMA waomba ulinzi Lissu arudi nchini
TAMISEMI yaridhishwa matumizi ya fedha ujenzi wa miradi Kinondoni