Ofisi ya takwimu taifa kwa kushirikiana na mtakwimu Zanzibar pamoja na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS imedhamiria kupunguza maambukizo mapya ya virusi vya ukimwi mpaka kufikia 2030.

Mkurugenzi mkuu ofisi ya takwimu Taifa Dkt. Albina Chuwa  amesema wanatarajia kufanya utafiti wa kiwango cha mambukizi ya virusi vya ukimwi ,uelewa na upatikanaji wa madawa ya kupunguza makali na maambukizi mapya.

chuwa

Aidha Dkt Chuwa amesema kuwa upimaji wa sasa utapima kuanzia mtoto mchanga mpaka watu wazima tofauti na hapo awali ambapo kulikuwa na changamoto ya vifaa na wataalamu.

Hata hivyo Dkt. Chuwa amewataka wananchi kutoa ushirikiano ili serikali iweze kupata takwimu sahihi na bora ili kupanga mipango ya maendeleo kwa wananchi wake hasa  walioathirika na ugonjwa wa ukimwi.

Mkurugenzi mtendaji TACAIDS Dr. Fatma Mrisho amesema lengo la ulimwengu ifikapo 2030 ni kufikisha sifuri tatu yaani kutokuwepo na vifo vitokanavyo na ukimwi, unyanyapaa kwa waathirika na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.

Hata hivyo Dk. Mrisho asisitiza kwamba ukimwi bado upo na unaathiri maendeleo ya nchi hivyo kama tume ya kudhibiti maambukizi wana lengo la kuhakikisha 90%ya waathirika wanajitambua na kutumia dawa  ili kuepusha maambukizi mapya yasiyo na sababu ifikapo 20120.

mrisho

Pamoja na hayo Dkt. Chuwa amesema kuwa utafiti wa sasa ni wanne nchini ambapo utafanyika kwa miezi miwili na kusema kuwa unatarajiwa kuanza juni mwaka huu ,ambapo utafiti wa kwanza nchini  kiwango cha maambukizi kilikuwa 7.0%, na awamu ya pili ilikuwa 5.75 % na 5.1% .

Hans Poppe: Hakuna Mchezaji Wa Kigeni Aliyeachwa Simba
Wabunge wa Ukawa, CCM wamgomea Naibu Spika kukataa hoja ya wanafunzi waliofukuzwa UDOM