Michezo ya mabunge ya Afrika Mashariki inatarajia kuanza kutimua vumbi Desemba 03 mwaka huu katika viwanja vya taifa na Uhuru jijini Dar es Salaam.

Michuano hiyo inayoshirikisha mabunge kutoka katika mataifa sita ya Afrika Mashariki na Tanzania ikiwa mwenyeji kwa mwaka huu.

Michezo itakayohusika katika mashindano hayo ni pamoja na soka, netiboli, riadha, kuvuta Kamba, wavu pamoja na mchezo wa kutembea kwa mwendokasi.

Mwenyekiti wa timu hiyo, ambaye ni mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, amesema bunge la Tanzania limejipanga kutwaa ubingwa katika michezo yote na limeandaa wanamichezo takriban 102 ambao ni wabunge pamoja na watumishi wa bunge na kwa sasa wanaendelea na mazoezi katika kituo cha michezo cha Jakaya Kikwete, Kidongo Chekundu Dar es Salaam.

Amesema viongozi wakuu wa nchi akiwemo Rais, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais, Spika wa Bunge ambaye ndiye mwenyeji pamoja na Naibu Spika pia watapata fursa ya kushiriki michezo hiyo kwa namna mbalimbali.

 

Zimbabwe Warriors yajitoa kombe la Challenge
Tiketi 742,760 za kombe la dunia zauzwa