Mamia ya watu wameandamana jijini Nairobi, Kenya kupinga mauaji ya kiholela ambayo yanadaiwa kutekelezwa na maafisa wa usalama nchini humo.

Waandamanaji hao wameanzia msafara wao eneo la Freedom Corner, uwanja wa Uhuru Park na kupitia katikati mwa jiji ambapo watafika pia makao makuu ya polisi na makao makuu idara ya mahakama.

kenya 1

Maandamano hayo yamefanyika kufuatia kupatikana kwa miili ya watu watatu ambao ni Wakili Willie Kimani, mteja wake Josephat Mwendwa na dereva wa teksi Joseph Muiruri.

Bw Kimani na Bw Mwenda walikuwa wamekodisha gari la Bw Muiruri baada ya kuhudhuria kesi katika mahakama ya Mavoko Juni23, walipotekwa na watu wanaodaiwa kuwa maafisa wa usalama.

Aidha miili yao ilipatikana katika mto wa Ol Donyo Sabuk, jimbo la Machakos, mashariki mwa jiji la Nairobi, ikiwa imefungwa mkono na ikionekana kuwa na ishara za majeraha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali la tume ya haki za Binadamu Kenya amesema kuwa mauaji ya vijana hawa watatu yanafaa kumtia wasiwasi Rais Kenyatta.

kenya pic

“Kiongozi wa nchi ni sharti aunde jopo la uchunguzi kuhusu kutekwa na kutumiwa vibayakwa idara za polisi na rasilimali zake kwa manufaa ya watu binafsi na katika kutekeleza uhalifu ikiwa ni pamoja na, katika kisa hiki, mauaji ya kiholela.”

Aidha chama cha Wanasheria Kenya kimewashauri wanachama wake kususia shughuli za mahakama kutokana na kuuawa kwa wakili mwenzao Bw, Kimani

Vile vile baadhi ya Mashirika ya kutetea haki za binadamu wanataka Mkuu wa Polisi Joseph Boinnet na Waziri wa Usalama Joseph Nkaissery wajiuzulu kutokana na tukio hilo.

Kwa mujibu wa shirika lisilo la kiserikali linalofuatilia visa vya ukatili wa polisi dhidi ya raia Kenya la IMLU, mwaka 2015 watu 125 waliuawa kiholela na maafisa wa polisi, huku kati ya january mpaka Aprili mwaka huu watu 53 wameuawa kwa mujibu wa IML.

Hata hiyo maaafisa watatu wa polisi wanaotuhumiwa kuhusika kutoweka kwa Bw. Kimani,Bw. Mwenda, Bw. Muiruri wapo chini ya uangalizi na walitarajiwa kufikishwa mahakamani leo.

Video: Magoli 50 yaliyogungwa kiufundi zaidi Duniani
Roma ataja siku ya kuiachia Video na Audio ya ‘Kaa Tayari’… kuyapekua matukio ya JPM?