Waziri Mkuu wa Lebanon Hassan Diab ametangaza kujiuzulu kufuatia maandamano makali ya wananchi baada ya mlipuko wa Beirut ambapo Rais Michel Aoun amekubaliana na hatua hiyo ya serikali kujiuzulu.

Baadhi ya mawaziri tayari walikuwa wamejiuzulu hapo kabla, kufuatia maandamano makubwa ya kuipinga serikali yaliyoibuka baada ya mlipuko huo kutokea.

Kwenye taarifa yake fupi kupitia televisheni, waziri mkuu Diab amesema anachukua hatua hiyo ili aungane na watu wa Lebanon na kwa pamoja wapiganie mabadiliko.

” Ninatangaza leo kujiuzulu kwa serikali hii. Mungu ailinde Lebanon”amesema Waziri Mkuu Diab

“ufisadi ndio chanzo cha janga hili, Kile kilichopo katikati yetu na mabadiliko ni ukuta mwembamba unaolindwa na mbinu chafu”ameongeza Diab

Ikumbukwe wiki iliyopita Diab alimlaumu mtangulizi wake kwa mlipuko huo ambapo alisema kuwa wanasiasa wanatakiwa kuona aibu kwa sababu ufisadi ndio umesababisha janga hilo lililofichwa kwa miaka saba.

Simba SC yawaita Young Africans mezani
WTTC waipa heshima Tanzania, Kigwangala aunguruma