Maneno hayo yamesemwa na Jeshi la polisi katika harakati za kufifisha na kukemea tukio la maandamano lililopangwa kufanyika Aprili 26 siku ambayo Watanzania wanaenzi Muungano wao baina ya Tanganyika na Zanzibar uliotiwa saini  na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Abeid Amani Karume.

Maandamano hayo yanahamasishwa na mwanadada, Mange Kimambi ambaye ni mwanaharakati kupitia mitandao ya kijamii mwenye ushawishi mkubwa ambapo ameunda makundi ya watu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania kufanya maandamano ya amani ifikapo tarehe hiyo yakiwa na lengo la kupinga mambo yanayoendelea nchini.

Hivyo jeshi la polisi kupitia kamishna wa Oparesheni na Mafunzo, Nsato Marijani ametoa onyo kali kwa kikundi kinachohamasisha maandamano ya kuiangusha Serikali kupitia mtandao wa Telegram ambapo amesema kitendo hicho ni sawa na uhaini.

Hivyoa amepiga marufuku maandamano hayo ambayo yapo kinyume na sheria, amesema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watu watakaovunja sheria.

“kitendo cha kufanya maandamano ukiwa na nia ya kuiondoa serikali ni Uhaini” amesema Nsato.

Mbali na jeshi la polisi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli jana katika uzinduzi wa tawi la benki ya CRDBMkoani Geita Wilayani Chato, ametoa onyo kali kufanyika kwa maandamano hayo na kusema watakaofanya maandamano hayo watakiona.

Mexime: Wachezaji wanafanya makosa mengi
Tillerson awapongeza Uhuru Kenyatta na Raila Odinga