Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya  Dini  zote Nchini, Askofu William Mwamalanga amesema kuwa jamii isimshambulie Rais Dkt. Magufuli kuhusu kauli yake kwa wanafunzi watakaopata mimba wakiwa shuleni.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam wakati akifunga kongamano la siku mbili  lililoshirikisha vijana  2783 kutoka  wilaya za Tanzania Bara ambao ni wajumbe wa kueneza Maadili na Amani vijijini kupitia mpango maalumu wa kuwafikia vijana kujiepusha na maadili hatarishi ya matumizi ya dawa za kulevya na kupinga elimu ya ugaidi kwa vijana wote nchini.

“Kumshutumu Rais Dkt. Magufuli ni kitendo cha kulea  majambazi wa ubakaji na ndoa za utotoni, hapa ni lazima Serikali iweke ulinzi kwa wanafunzi wa kike wanaosoma shule za mbali na makazi ikiwa ni pamoja na kuwapima wasichana wote wakati shule zinaanza kwa kila muhula wa masomo”, amesema Askofu Mwamalanga.

Hata hivyo, Mwamalanga ameongeza kuwa kwa hilo Rais Dkt. Magufuli yupo sahihi kwa asilimia 100 kwa zambi dawa yake ni kuikata kwa macho meupe.

Kubenea asomewa shitaka la kumshambulia mbunge
IGP Sirro apokea msaada wa magari