Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo kwenye baraza la mawaziri.

Katika mabadiliko hayo Rais Samia amemteua Dkt. Stergomena Tax kuwa waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akichukua nafasi ya Balozi Liberata Mulamula.

Innocent Bashungwa ameteuliwa kuwa waziri wa Ulinzi nafasi iliyokuwa ya Dkt. Stergomena.

Pia amemteua Angela Kairuki kuwa Mbunge na kuwa waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Aidha haijatajwa Balozi Liberata Mulamula sababu za kutoka nje ya Wizara aliyokuwa akiitumikia na wateuliwa wote wataapishwa Octoba 3 ikulu ya Dar es Salaam.

Habari kuu kwenye magazeti ya leo Octoba 03, 2022
Ghasia uwanjani zauwa 174 hasira timu kufungwa nyumbani