Wajumbe saba kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), wametangazwa hii leo baada ya kikao maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema ameteuliwa kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa, akichukua nafasi ya Shaka Hamdu Shaka.

Katikw Kikao hicho kilichofanyika hii leo Januari 14, 2023 na kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan, aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka amesema Kamati kuu ya CCM iliketi na vikao vyote vilihitimishwa chini ya mwenyekiti wake kwa kutangaza safu mpya za wajumbe wa NEC na kuidhinisha sekretarieti.

Nafasi za wajumbe kutoka Bara ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, Mwenyekiti wa CCM Tabora, Hassan Wakasuvi na aliyewahi kuwa katibu Mkuu wa umoja wa wanawake Tanzania, Halima Mamuya.

Aidha, kwa upande wa Zanzibar ni Mohamed Abood Mohamed, Injinia Nasri Ally na Leyla Burhan Ngozi ambapo kila upande ulikuwa na nafasi mbili za wanaume na nafasi mbili wanawake ambapo pia kikao hicho kimeithibitisha sekretariet ya Halmashauri kuu ya taifa na kutaja orodha ya wajumbe waliochaguliwa.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa, Sophia Mjema.

Shaka amesema, nafasi ya Katibu Mkuu itaendelea kushikiliwa na Daniel Chongolo, Naibu Katibu Mkuu Bara, Annamringi Macha na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Mohemed Said Dimwa ambapo pia amesema, Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha ni Dkt. Frank Hawasi, Katibu siasa na uhusiano wa kimataifa ni Mbarouk Nassoro na Katibu wa Oganaizesheni niIssa Haji Usi Gavu.

Aidha mbele ya Waandishi wa Habari Shaka amesema kwamba, “Nawashukuru Wanahabari kwa namna ambavyo tulifanya kazi pamoja, niwaombe tumpe ushirikiano Dada yangu Sophia Mjema, Chama chetu ni chema.”

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 15, 2023
Mamlaka yatoa nauli mpya Mwendokasi, Taxi