Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi amefanya mabadiliko ya Baraza lake la Mawaziri, kwa kumteua aliyekuwa Makamu wa Rais wa nchi hiyo Jean-Pierre Bemba kuwa waziri wa ulinzi.

Bemba, kiongozi wa zamani wa waasi alikamatwa mwaka 2008 na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita na uhalifu dhidi ya binadamu uliofanywa na wanajeshi wake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kati ya mwaka 2002 na 2003.

Kupitia taarifa iliyorushwa na Luninga ya Taifa la DRC, imeeleza kuwa uteuzi huo, ni sehemu ya mabadiliko makubwa ya maafisa 57 wa serikali, ambayo msemaji wa rais alisema ni ya haraka na lazima.

Jean-Pierre Bemba (kushoto), akiwa na Vital Kamerhe. Picha ya Umuseke.

Tshisekedi, pia amemteua Mkuu wake wa zamani wa utawala, Vital Kamerhe ambaye aliachiliwa kutoka gerezani mwezi Desemba 2021, baada ya kupatikana na hatia ya ubadhirifu wakati alipokuwa waziri wa Fedha.

Hata hivyo, mabadiliko hayo makubwa zaidi kuliko ilivyotabiriwa, yanakuja ikiwa ni kabla ya uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika Desemba 20, 2023, ambapo Tshisekedi anatarajiwa kuwania muhula wa pili.

Serikali yataka Wananchi kutumia fursa, kufanya kazi kwa bidii
Panya atumika kubaini vijidudu ugonjwa Kifua Kikuu