Uongozi wa Uwanja wa Benjamin Mkapa umeendelea kulia na matumizi mabaya ya Miundombinu ya Uwanja huo hususan maeneo ya Maliwato.

Meneja wa Uwanja huo Mkubwa kuliko viwanja vyote vya michezo nchini Tanzania, Gordon Nsajigwa amesema Mashabiki wa soka wanaojitokeza mara kwa mara uwanjani hapo kwa ajili ya wamekua na tabia ya kushindwa kutunza Miundombinu ya Maliwato.

Amesema baada ya Matamasha ya Siku ya Mwananchi na Simba Day, Sehemu za Maliwato za Uwanja huo zimeachwa katika hali ya uchafu, jambo ambalo ni aibu kwa kila mmoja aliyefika Uwanjani hapo.

“Imekua kasumba kwa kila michezo mikubwa inayofanyika hapa Mashabiki wanashindwa kutunza sehemu za Maliwato, kitu ambacho ni aibu kwa kila anayefika hapa”

“Baada ya Matamasha ya timu kubwa (Simba na Yanga) Miundombinu ya Maliwato imeachwa katika hali ya uchafu na tumekua tukijitahidi kuhakikisha inakua safi mara zote lakini Mashabiki hawatoi ushirikiano wa kutosha kwa Uongozi wa Uwanja.”

“Kuna haja ya Serikali kuendelea kuutunza Uwanja huu, pia Mashabiki wana kila sababu ya kubadilika kwa sababu hiki kitu ni cha kwao na wanapaswa kuchungana wao kwa wao ili kutunza mazingira ya Uwanja wetu” amesema Nswajigwa

Wakati huo huo imeelezwa kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi kumpangia majukumu mengine Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa Godon Nsajigwa.

Taarifa iliyotolewa na Abbasi inasema kuwa Meneja huyo anapangiwa majukumu mengine kwa kushindwa kusimamia matumizi endelevu ya Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Akieleza utekelezaji wa agizo hilo, amesema tayari taratibu zimekwishaanza za kupangiwa majukumu mengine na nafasi hiyo inatarajiwa kujazwa mara moja.

Tanzania kuendelea kula neema za FIFA
Mbunge mbaroni kwa kumshambulia mpiga kura.