Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limetoa maagizo ya kusitishwa kwa mchakato wa mabadiliko ya umiliki wa klabu za wanachama.

Agizo hilo la serikali linagusa umiliki wa hisa na ukodishwaji, hadi marekebisho ya katiba yatakapofanyika kwa mujibu wa sheria ya Baraza la Michezo la Taifa na kanuni za Msajili namba 442 yatakapofanyika.

Akitangaza taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari kaimu katibu mkuu wa Baraza la michezo Tanzania Mohamed Kiganja amesema Serikali inapenda klabu hizo zifanye mabadiliko ya kimfumo lakini zinapaswa kufuata utaratibu.

“Baraza linapenda kuona wahusika wanafuata sheria na taratibu za nchi katika kufikia malengo yao. Kuendelea na mchakato huu kabla ya taratibu za kurekebisha katiba zao kisheria ni kosa na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya watakaokiuka maelezo haya.” Alisema Kiganja

BMT imeshauri wadau wote wanaotaka kumiliki klabu ya michezo kuanzisha timu zao kama Said Salim Bhskressa alivyoamua kuanzisha Azam FC.

Manuel Neuer: Schweinsteiger Anaweza Kutoa Msaada
Guardiola Aridhia Kumtoa Sadaka Silva, Amuhusudu Julian Weigl