Chama cha soka nchini England FA, kimeziadhibu klabu za Chelsea pamoja na West Ham Utd, kufuatia utovu wa nidhamu uliojitokeza wakati wa mchezo uliozikutanisha klabu hizo mbili mwezi uliopita.

FA, wamezitoza faini klabu hizo za magharibi mwa jijini London ya pauni elfu 40 na 50, baada ya kuonekana wakuu wa benchi la ufundi wa pande zote mbili walishindwa kuwahimiza wachezaji wao kuwa na nidhamu wakati wote wa mtanange huo, ambao ulimalizika kwa Chelsea kubanjuliwa mabao mawili kwa moja.

Wachezaji watano wa Chelsea walionyeshwa kadi za manjano huku kiungo Nemanja Matic, akiadhibiwa kwa kadi nyekundu na meneja Jose Mourinho aliamuriwa kuondokwa kwenye benchi la ufundi na kwenda kukaa jukwaani.

Kwa upande wa wachezaji wa West Ham Utd wameingizwa kwenye mlolongo huo wa adhabu ya kupigwa faini, kutokana na kitendo cha kumzonga muamuzi, Jonathan Moss, kwa kumshurutisha ili amuwajibishe Matic kutokana na madhambi aliyokua amemfanyia mshambuliaji wa The Hammers, Diafra Sakho katika dakika ya 44.

Kama hiyo haitoshi wachezaji wa Chelsea walionyesha utovu wa nidhamu kwa mara ya pili kwa kumzonga muamuzi baada ya kumuadhibiwa Matic.

Maalim Seif: Msikubali Kuchokozwa
Kikwete: Taifa Stars Mpeni Heshima John Magufuli