Mabalozi wateule, wanaokwenda kuwakilisha Tanzania nchi za Zimbabwe, Zambia na Uholanzi, wametakiwa kuitumia vyema Diplomasia ya Kiuchumi kwa kuzitafuta fursa mbalimbali za kibiashara na kuzileta nchini Tanzania.

Wito huo, umetolewa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi, Simon Sirro anayekwenda Zambia, Balozi, Luten General Metheu anayekwenda Zimbawe na Balozi, Caroline Chipeta anayekwenda nchini Uholanzi.

Serikali yawageukia Wafanyabiashara wa Mkaa

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman (mwenye tai nyekundu), akiwa katika Picha ya pamoja na Balozi Mteule wa  Tanzania nchini Zambia, IGP Mstaafu Saimon Sirro na Balozi wa Tanzania Nchini Uholanzi Cathrene Chipate (kulia), na Balozi wa Tanzaia nchini Zimbabwe, Luteni General Methew Kingule (kushoto). 

Amesema, katika nchi wanazokwenda zipo fursa nyingi za kiuchumi na kiutaalamu ambazo zinaaweza kuisaidia Tanzania kujiendeleza zaidi, iwapo mabalozi hao watafanya juhudi ya kuzileta nyumbani ili kusaidia nchi yao.

Othman amewaeleza Mabalozi hao kuwa, Tanzania zipo fursa nyingi za kuchumi za kukuza na kuendeleza sekta ya utalii , biashara na kilimo maeneo ambayo hayajatumika ipasavyo hivyo mabalozi hao wajitahidi kuitumia nafasi hiyo.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman (kulia), akizungumza na Mabalozi wateule wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania nje ya nchi. wa kwanza (kushoto), ni Mkurugenzi wa idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Marriam Haji Mrisho. 

Akiongea wakati wa mkutano huo, Kiongozi wa Mabalozi, IGP Mstaafu Simon Sirro amesema maelekezo wanayoyapata kutoka kwa viongozi wakuu ni nyenzo muhimu katika kazi yao na kwamba watajitahidi kuyatumia na kuyafuata ili kuiwakilisha vyema nchi.

Ameongeza kuwa, yeye na wenzake watajitahidi kuhakikisha wanafanya wajibu wao vizuri wa kuitangaza nchi na kushirikiana na watangulizi wao kupitia Diplomasia ya kiuchumi na kukidhi matarajio ya taifa kimaendeleo.

Habari kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 23, 2022
Serikali yawageukia Wafanyabiashara wa Mkaa