Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, (UDART) imesitisha huduma zake kwa baadhi ya njia kuanzia saa 11:00 alfajiri tarehe 15/04/2018 kutokana na kufungwa kwa Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kwa sababu ya mafuriko yaliyosababisha maji kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi.

Aidha, kwa sasa huduma zinatolewa kwa njia za Kimara – Morroco, Kimara – Magomeni Mapipa, na Gerezani – Muhimbili. Huduma kamili zitarejea mara baada ya barabara kufunguliwa.

Hata hivyo, Kampuni hiyo kupitia kwa mkuu wa kitengo cha mawasiliano, Deus Bugaywa imeomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

 

Fatma Karume aeleza atakachokipigania zaidi
Monalisa atwaa tuzo nchini Ghana