Kampuni inayosimamia huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam, UDA Rapid Transit (UDA-RT) inaujulisha umma kuwa huduma za mabasi hayo kwa baadhi ya njia zimesitishwa kuanzia leo Ijumaa, Mei, 04, 2018 mpaka pale taarifa kamili itakapotolewa.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART imeeleza kuwa sababu ya usitishwaji huo kuwa ni kutokana na kufungwa kwa barabara ya Morogoro eneo la jangwani kwa sababu ya mafuriko yaliyosababisha maji kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi.

Amesema kwa sasa huduma zinatolewa kwa njia ya Mbezi – Kimara, Kimara- Morroco, Kimara – MagomeniMapipa, Kivukoni – muhimbili, Gerezani- KivukoninaGerzani- Muhimbili.

Aidha ameomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza huduma kamili itarejea mara baada ya njia hizo kufunguliwa.

Video: Mtoto apata ugonjwa wa ajabu
Acha watunyooshe tu maana tulizoea kuropoka- Lucy Mayenga