Fedha za uwezeshaji zilizotolewa kwa ajili ya wananchi wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne iliyoongozwa na Dk. Jakaya Kikwete zilizobatizwa jina la ‘Mabilioni ya Kikwete’ zimeanza kuchunguzwa.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imeeleza kuwa imeanza kuzichunguza fedha hizo baada ya kudaiwa kuwa kati ya shilingi bilioni 50 zilizotolewa kwa ajili ya kukopeshwa wananchi kupitia vikundi mbalimbali, ni shilingi bilioni 43 pekee zilizorudishwa na kiasi cha bilioni 7 kimeliwa na ‘wajanja’.

Msemaji wa Takukuru, Tunu Mleli aliwaambia waandishi wa habari kuwa wameamua kuanza kuzichunguza tuhuma hizo kwakuwa ni jukumu lao kufanya hivyo. Mleli aliwataka wananchi wenye ushahidi wowote kuuwasilisha Takukuru ili uweze kusaidia katika uchunguzi huo.

Mikopo ya fedha hizo ilitolewa kupitia benki za CRDB, NMB, Community Bank na Benki ya Posta Tanzania.

Kangi Lugola amtega Rais Magufuli
Papa Wemba Afariki, Aanguka Jukwaani Mbele ya Maelfu