Mabingwa wa soka nchini Italia Juventus wamethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo kutoka Ujerumani Emre Can.

Juventus wamethibitisha taarifa za kumsajili Can, kwa mkataba wa miaka minne, baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Liverpool ya England aliyoitumikia kuanzia mwaka 2014.

“Klabu ya Juventus inatangaza kukamilisha usajili wa kiungo Emre Can, amesaini mkataba wa miaka minne ambao utaanza rasmi Julai Mosi.” Inasomeka taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Juventus.

Can mwenye umri wa miaka 24, anaondoka Liverpool baada ya kuitumikia klabu hiyo katika michezo 167, huku mchezo wake wa mwisho ukiwa wa hatua ya fainali, ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Real Madrid mwezi Mei.

Can, ambaye ameshaitumikia timu ya taifa lake la Ujerumani katika michezo 20, msimu uliopita wa 2017/18 aliicheza michezo 38 akiwa na Liverpool na kufanikiwa kufunga mabao sita, lakini hakujumuishwa kwenye kikosi cha timu yake ya taifa inayoshiriki fainali za kombe la dunia zinazoendelea nchini Urusi.

Habari kubwa katika magazeti ya leo Juni 22, 2018
Askofu Polycarp Pengo apata mrithi