Kikosi cha vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC kimeondoka mkoani Singida kuelekea Jijini Dodoma, kwa lengo la kuhudhuria shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa siku ya kesho Mei 14, 2018.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari na kusema ni kweli wamepewa mualiko wa kutembelea Bunge siku ya Jumatatu.

“Kikosi kinaelekea Jijini Dodoma kwaajili ya kuitikia wito wa mualiko tuliyopewa na Ofisi za Bunge kwa maana kutembelea Bunge siku ya kesho,”amesema Manara

Hata hivyo, kikosi cha Simba kinatinga Bungeni ikiwa ni kama sehemu ya kupongezwa kwa kazi nzuri waliyoifanya katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

 

Kingwangalla akabidhi magari 6 kwa wabunge
Barua ya maombi ya kazi itakayomshika muajiri wako

Comments

comments