Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Hispania Vicente del Bosque, ametaja kikosi cha wachezaji 26, kwa ajili ya maandalizi ya fainali za Euro 2016 zitakazofanyika nchini Ufaransa kuanzia mwezi ujao.

Del Bosque, amewaacha midimo wazi baadhi wa wadau wa soka nchini Hispania na kwingineko, kufutia maamuzi aliyoyachukua ya kumuacha washambuliaji Fernando Torres (Atletico Madrid), Diego Costa (Chelsea) pamoja na viungo Juan Mata (Man Utd), Santi Cazorla (Arsenal).

Kuachwa kwa wachezaji hao wane ambao alidhaniwa huenda wangekuwa sehemu ya kikosi cha mabingwa hao watetezi, kunadhihirisha kwamba, uwezo wao haukumridhisha Del Bosque wakati wote wa msimu wa 2015-16.

Kikosi kamili kilichotajwa na kocha huyo, upande wa makipa yupo Casillas, De Gea na Rico

Mabeki: Ramos, Pique, Carvajal, Alba, Bartra, Azpilicueta, San Jose, Juanfran

Viungo: Bruno, Busquets, Koke, Thiago, Iniesta, Isco, Silva. Pedro, Fabregas, Saul

Washambuliaji: Aduriz, Nolito, Morata, Vazquez

Kikosi cha Hispania, kitachea michezo mitatu ya kujipima nguvu kabla ya kuelekea nchini Ufaransa kutetea taji la Euro, ambapo watapambana na Bosnia and Herzegovina mnamo Mei 29 na kisha wachuana na Korea kusini na mpambano wao wa mwisho wa kujiweka sawa utashuhudia wakipapatuana na Georgia, Juni 07.

Katika mshike mshike wa Euro 2016, Hispania wataanza na jamuhuri ya Czech Republic (Juni 13), kisha Juni 17 watacheza dhidi ya uturuki na kumazia na

Croatia mnamo juni 21 kabl ya kufahamu hatma yao ya kufuzu hatua ya mtoano.

Kafulila apigwa chini rasmi, Mahakama yamhalalisha Mwilima
Kikosi Cha Mabingwa Wa Dunia Chaanikwa Hadharani

Comments

comments