Mabondia wa kulipwa wameruhusiwa kushiriki kwenye mashindano ya Olimpiki mwaka huu jijini Rio de Janeiro, Brazil baada ya chama cha ndondi cha kimataifa, AIBA kukubali kubadilika kwa katiba.

Mabondia wa kulipwa akiwemo Floyd Mayweather wanaweza kushiriki kwenye mashindano ya Olimpiki mwaka huu

Rais wa AIBA, Ching-Kuo Wu alisema kubadilika kwa katiba ya AIBA kumepitishwa kwa asilimia 95 na wajumbe 84 kati ya 88. Hiyo inamaanisha kuwa mabondia wa kulipwa sasa wataweza kuwania medali kwa mara ya kwanza kwenye mashindano hayo yanayoanza Aug. 5.

Jumla ya mabondia 286 watashiriki kwenye mashindano hayo.

Bingwa wa zamani wa uzito wa juu Mike Tyson, aliyewahi kushinda medali ya dhahabu kipindi anacheza ngumi za ridhaa mwaka 1981 na 1982 kwenye Junior Olympic Games, ameikosoa hatua hiyo.

Mabondia waliowahi kushiriki mashindano hayo kabla ya kuingia kwenye ndondi za kulipwa ni pamoja na Muhammad Ali, Joe Frazier, George Foreman, Lennox Lewis, Oscar De La Hoya na Vladimir Klitschko.

Manji Achukua Fomu, Awavua Uanachama Walioenda TFF
Tanzania Yaporomoka Viwango Vya Ubora Duniani