Katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha elimu na kulea kizazi kijacho ambacho kitasaidia Taifa kufikia malengo ya kiuchumi na kimaendeleo, Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imejenga na kukabidhi vyumba viwili vya madarasa kwa Shule ya Msingi Kiziba iliyopo Kijiji cha Mwenegeza kata ya Nyakagomba, Wilayani na Mkoa wa Geita.

Akizungumza wakati wa kukabidhi madarasa hayo, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa GGML, Terry Strong Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Dorine Denis, “GGML inaamini kuwa wananchi wa Tanzania ndio mtaji mkubwa wa kampuni hii na siku zote imekuwa ikiunga mkono juhudi za serikali za kuboresha elimu na kujenga kizazi kijacho ambacho kitasaidia taifa la Tanzania kufikia malengo yake makubwa ya kiuchumi na kimaendeleo.

Madarasa yaliyokabidhiwa Shule ya Msingi Kiziba iliyopo Kijiji cha Mwenegeza kata ya Nyakagomba, Wilayani na Mkoa wa Geita.

Dorine ameongeza kuwa, “GGML imedhamiria kuchochea maendeleo endelevu ya jamii zinazozunguka mgodi na imedhihirisha hilo mara kwa mara kwa kushirikiana kikamilifu na serikali katika kuboresha huduma za jamii ikiwemo elimu, afya, maji na barabara pamoja na shughuli nyingine za kiuchumi kwa jamii zinazozunguka mgodi huo.”

Alisema GGML inafanya kazi ya kuunga mkono malengo ya serikali ya Tanzania ya ukuaji thabiti wa uchumi na maboresho ya miundombinu ya kijamii huku akiongeza kuwa, “hii inaendana na thamani yetu ya msingi ya kusaidia serikali katika kukuza ukuaji wa uchumi wa muda mrefu katika jamii tunakofanyia kazi. Kwa hiyo nimefurahishwa kwamba ujenzi wa madarasa haya umetokana na juhudi za ushirikiano kati ya serikali, jamii mwenyeji na GGML,” alisema.

Burudani wakati wa uzinduzi wa madarasa mawili yaliyojengwa na kampuni hiyo katika Shule ya Msingi Kiziba iliyopo Kijiji cha Mwenegeza wilayani Geita.

Aidha, aliahidi kuwa GGML itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania na wadau wengine ili kufikia lengo la sekta ya madini la kuchangia asilimia 10 katika pato la taifa ifikapo mwaka 2025 huku Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Kiziba, Beatus Mwandu aliishukuru GGML kwa ujenzi wa madarasa hayo hasa ikizingatiwa shule hiyo bado inakabiliwa na uhaba wa madarasa huku mengine yakiwa yamechakaa.

Naye, Mtendaji wa Kata ya Nyakagomba, Christopha Amos naye aliishukuru GGML kwa msaada huo na kuahidi pia kufikisha kilio cha changamoto nyingine kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita ili azifanyie kazi.

Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Kiziba, Beatus Mwandu aliishukuru GGML kwa ujenzi wa madarasa hayo yaliyokabidhiwa Dorine akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa GGML, Terry Strong, mbele ya Mtendaji wa Kata ya Nyakagomba, Christopha Amos. (Wote hawapo pichani).

Madarasa hayo mawili yenye thamani ya Shilingi milioni 42, yanalenga kusaidia kutoa mazingira mazuri ya kujifunzia kwa wanafunzi ambao ufaulu wao umeathiriwa na mazingira magumu ya kujifunza.

Tanzania, UAE zasaini ushirikiano utunzaji wa Mazingira
Serikali yasisitiza matibabu bure kwa watoto