Mtandao maarufu wa Instagram umefanya maboresho mapya ambapo watumiaji wa mtandao huo kwa sasa atakuwa na uwezo wa kuweka (ku-post), kupandisha (ku-upload) video na picha katika akaunti zao za Instagram kwa kupitia tovuti/website ya Instagram.

Hata hivyo maboresho hayo yanatarajiwa kuwa na msaada kwa watu wengi hasa wanaosimamia akount za watu ambao wanatumia Kompyuta katika shughuli mbalimbali na kupunguza matumizi ya simu.

Feature hii imeanza kutumika wiki hii kwa baadhi ya watumiaji na itaendelea kutoka taratibu kwa watumiaji wengine.

Kwa sasa feature ya kupandisha video zinazozidi sekunde 60 (zaidi ya dakika moja) inayofahamika kama IGTV imeondolewa na badala yake mtumiaji ata weka video ndefu na fupi kwenye feature moja ya VIDEOS.

KMC FC kibaruani tena kesho
Madeni kwa Serikali yaikwamisha PSSSF