Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe mapema leo hii amesema mabosi wa kampuni moja iliyopo Mwanza waliowahi kufanya kazi na msanii wa maigizo ya Vichekesho King Majuto na kumtapeli kiasi cha pesa milioni 24 wamewekwa rumande kwa kuhujumu nguvu kazi ya msanii huyo.

Amesema kuwa King Majuto aliwahi kuingia mkataba na kufanya kazi na kampuni hiyo ambayo ilimdhurumu kiasi cha milioni 24 waliodai kumlipa kwa kazi hiyo, na mwisho wa siku kumkabidhi cheki ya gharama hiyo isoyokuwa na kiasi hiko cha pesa.

”Lakini tayari kuna kampuni moja ya Mwanza waliingia mkataba na king Mahjuto mkataba huo ulikuwa wa kumlipa Bilioni 24 wakatoa cheki , cheki ikawa haina pesa benki, nashukuru sana uongozi wa Mwanza kwa  kushirikiana nao na wahusika wapo ndani na tutaendelea kuchukua hatua kali, kali kweli kweli kwa watu ambao wanadhani wanaweza kutumia jasho la wenzao kujinufaisha wenyewe,” amesema Mwakyembe.

Amesema tayari ameunda jopo la wanasheria na wameshakaa kikao cha kwanza ambapo wamekubaliana kupitia mikataba yote ya Mzee Majuto na kisha kuwaandikia barua makampuni yaliyofanya kazi na Majuto kupitia upya mikataba hiyo.

”Nimeunda jopo la wanasheria tumeshafanya kikao cha kwanza na sababu tumeanza na swala la majuta kazi yetu yetu kubwa ni kuangalia kazi zote ambazo wamekwisha zifanya na tunawaandikia barua wote waliohusika watupe mikataba wanaoijua wao tutakaa nao tuweze kuchambua mkataba  mmoja baada ya wengine” Mwakyembe.

Aidha amesema taarifa kamili itatolewa juu ya kile kitachokuwa kinaendelea na kitakachobainika katika mchakato huo, amesisitiza hatua kali kuchukuliwa dhidi ya hao wadhulumishi wa haki za wasanii, kama kiongozi wa Wizara hiyo ameahidi kusimamia kinagaubaga mchakato huo.

Hata hivyo Mzee Majuto tayari safari yake imekwishafanikishwa yupo nchini India Mumbai kwa ajili ya matibabu ya kidonda alichofanyiwa upasuaji wa tezi dume mwezi Januari mwaka huu.

 

Seneta afikishwa mahakamani akiwa kwenye kitanda cha wagonjwa
Ndalichako aagiza Nacte na TCU kuvifungia vyuo visivyokidhi vigezo