Aliyekuwa Mbunge wa Kasulu kwa tiketi ya chama cha NCCR-Mageuzi Moses Machali amesema kuwa  Rais Dk. John  Magufuli anatakiwa kuongeza kasi ya utumbuaji majipu kwa watumishi wa umma ili kuweka nidhamu ya uwajibikaji.

Machali amesema ya kuwa Rais Magufuli pamoja na kuwatumbua vigogo wakubwa na wengine kufikishwa kwenye vyombo vya dola, lakini bado ni mpole, anatakiwa aongeze kasi na ikiwezekana  afanye kazi kama kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un au kama kiongozi wa Ufilipino Rodrigoz Durtete.

“Dkt. Magufuli bado mpole lakini vichwa wacha viliwe,taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Mkuu wa Hesabu za Serikali,(CAG) zinaonyesha ni jinsi gani fedha za Serikali zinavyoliwa,Rais awe kama Rais wa Korea Kaskazini au wa Ufilipino,” amesema Machali.

Amesema Tanzania inahitaji kuwa na rais mkali kama walivyo marais wa  nchi za Korea Kaskazini na Ufilipino, ambao wanafanya kazi usiku na mchana huku wakisimamia sheria kali za nchi kwa kuwabana mafisadi na wala rushwa kwa kutoa hukumu kali ambazo ni fundisho.

 

 

Asha Baraka: Najipanga kuwaachia vijana muziki wa dansi na kuingia kwenye siasa
Wema Sepetu, Rapper Future wauanza mwaka kwa style moja