Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla, ameongeza siku 12 kwa wafanyabiashara wadogo (wamachinga) kuhama katika maeneo yasiyo rasmi wanayofanyia biashara ili kila mmoja aweze kwenda katika eneo atakalokuwa amepangiwa.

Makalla ametoa uamuzi huo leo Oktoba 18, mwaka huu wakati alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara wa Kariakoo kuhusu mpango wa kuwaondoa katika sehemu zisizo rasmi, huku akiwataka wafanyabiashara hao kuzingatia muda ulioongezwa na baada ya hapo hatataka kusikia kisingizio chochote.

“Nawapa muda mpaka Oktoba 30, baada ya hapo sitaki kusikia kisingizio chochote labda mtu aje na malalamiko kwamba kaenda kwenye maeneo yaliyotengwa kakosa nafasi,” amesema Mkuu huyo wa Mkoa.

Makalla ametaja maeneo ambayo wafanyabiashara hao wanatakiwa kuondoka kuwa ni kwa wale walio juu ya mifereji na mitaro kwenye hifadhi za barabara na mbele ya shule za Serikali au taasisi za Serikali.

Wakazi achefukwa na vita ya Machwa wa Diamond na Harmonize
Mmarekani mweusi wa kwanza kuwa waziri masuala ya kigeni afariki dunia