Wafanyabiashara wadogo zaidi ya 2000 wanaotembeza na kuanika pembeni ya barabara biashara zao maarufu kama Machinga wamepigwa marufuku jijini Dar es Salaam kuanzi jana.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi amesema kuwa tayari utaratibu wa kuwapangia maeneo katika masoko rasmi umekamilika na kwamba kuanzia kesho hawatatakiwa kuonekana wakifanya biashara zao katika eneo lolote tofauti jijini humo.

Alisema kuwa masoko rasmi yaliyotengwa ni pamoja na Kigogo Fresh lililopo eneo la Pugu, Ukonga karibu na gereza, Tabata Muslim na Kivule ambayo wafanyabiashara hao maarufu kama wamachinga wanatakiwa kwenda.

Mgurumi alieleza kuwa zoezi la kuwatambua lilikamilika lakini licha ya kupata machinga 2000, wameandaa maeneo ya masoko yanayoweza kuwapa nafasi zaidi ya wafanyabiashara hao 6000.

Aidha, alisema kuwa mbali na kuondoa machinga, kesho operesheni itakayoanza itahusisha pia wenye gereji ‘bubu’.

“Kwa hiyo sitarajii kuona watu maeneo hayo kesho, operesheni hii itaenda sambamba na kuwaondoa wenye gereji bubu na wanaoosha magari,” anakaririwa.

Mama Salma Kikwete amkingia kifua mumewe, ataka asilinganishwe
Mwanafunzi avuruga mabilioni baada ya benki kumuwekea kimakosa bilioni 10, kilichomtokea...