Wafanyabiashara wadogo maarufu kama Machinga wamezua kizaazaa katikati ya mji wa Morogoro baada ya kufunga baadhi ya barabara na kutandika bidhaa zao kwa lengo la kujipatia wateja katika msimu huu wa sikukuu.

Baadhi ya wananchi wameeleza kuhofia usalama wa mali zao wanapopita katika barabara zilizofurika wafanyabiashara na wanunuzi wa bidhaa hizo, hivyo kuiomba Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuwaondoa katikati ya mji na kuwahamishia katika maeneo maalum yaliyotengwa.

Kutokana na kilio hicho cha baadhi ya wananchi, Mkurugunzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, John Mgalula amesema kuwa halmashauri hiyo inapanga kuwaondoa wafanyabiashara hao katikati ya mji na kuwapeleka kwenye maeneo waliyotengewa.

Alisema ili kufanikisha hilo, amepanga kukutana na viongozi wote wa Halmashauri hiyo kuweka mkakati wa namna bora ya kuwaondoa wafanyabiashara hao katikati ya mji huo.

Machinga walianza kuonekana zaidi katikati ya miji mingi nchini kufuatia agizo la Rais John Magufuli kuwataka wakuu wa wilaya kutowanyanyasa wafanyabiashara wadogo kwa kuwapeleka maeneo ya mbali ya mji ambako hawatafanya biashara zao vizuri kutokana na kuwa mbali na wateja husika.

Wafugaji watishia kuchukua maamuzi magumu
Dkt. Shein azipongeza Cuba na Oman