Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi leo, Jumatatu wamezindua mtambo wa umeme jua katika eneo la Mirzapur katika Jimbo la Uttar Pradesh.

Uzinduzi huo umekuja siku moja baada ya viongozi hao wawili kwa pamoja kuwa wenyeji wa maonyesho ya kimataifa ya vifaa vya umeme jua yaliyofanyika jijini New Delhi.

Mbali na Macron na Modi, maonyesho hayo pia yalihudhuriwa na wakuu wa nchi mbalimbali duniani.

Umoja wa Kimataifa wa Solar ni mkataba wa chombo cha kimataifa ambacho kinatumika kuhamasisha matumizi bora ya nishati ya jua ili kupunguza matumizi ya nishati itokanayo na mafuta ambayo ina athari kimazingira.

Chombo hicho kilizinduliwa kwa pamoja kati ya India na Ufaransa kando mwa Mkutano wa Hali ya Hewa uliofanyika jijini Paris mwaka 2015.

Macron aliwasili nchini India Ijumaa iliyopita kwa ziara ya siku nne.

Ndege ya Bangladeshi yalipuka na kuua 50
Mkutano wa Korea Kaskazini na Marekani wasubiriwa kwa hamu