Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron ametaka kufanyika kwa mkutano wa haraka wa Umoja wa Ulaya kujadili mustakabali wa bara hilo kutokana na hali ya mambo inavyokwenda.

Ameyasema hayo wakati wa mkutano uliofanyika mjini Athens nchini Ugiriki, ambapo  Macron ameonya kuwa Ulaya itakufa endapo haitafungua milango ya mijadala kwa wananchi.

Macron amesema kuwa viongozi wa Ulaya wanapaswa kuwasilisha mapendekezo yao ifikapo mwishoni mwa mwaka huu yatayofungua mjadala kwa wananchi kuamua ni aina gani ya muungano wanaouhitaji.

Hata hivyo, Rais huyo wa Ufaransa ameahidi kuwasilisha mapendekezo yake ndani ya wiki chache zijazo, huku akisema itahusisha njia za kidemokrasia zaidi ikiwemo bunge la nchi yake.

Video: Lissu alivyoponea tundu la sindano, Mawaziri wang'oka
Maaskofu waamua kurudisha fedha za Escrow