Rais wa ufaransa Emmanuel Macron ametembelea nchi ya lebanon saa chache tu baada ya viongozi kumteuwa Mustapha Adib, mwanadiplomasia mwenye umri wa miaka 48, kuwa waziri mkuu mpya na mwenye jukumu la kuukabili mgogoro mkubwa wa nchi hiyo wa kisiasa na kiuchumi.

Macron Yuko Lebanon kwa ziara ya siku mbili iliyosheheni shughuli nyingi na mazungumzo ya kisiasa yanayolenga kuipa ufumbuzi nchi hiyo na baada ya kufika Mjini Beirut alikutana na mwanamuziki wa kike maarufu nchini humo Fairouz kwa shuguli binafsi kabla ya waziri mkuu mpya.

Kisha akakutana na waziri mkuu wa zamani Saad Hariri katika makazi ya balozi wa Ufaransa. Akizungumza katika uwanja wa ndege wa Beirut, Macron alitoa wito wa kuundwa haraka serikali mpya ya Lebanon kufuatia kuteuliwa kwa waziri mkuu mpya.

” Nimeona mchakato umeanza katika saa chache zilizopita ambao umewezesha kupatikana kwa waziri mkuu. Sio jukumu langu kumuidhinisha au kumbariki – ni uhuru wa Walebanon ambao ndio suala la msingi hapa – Lakini uhakikishe kuwa serikali yenye lengo inaundwa haraka iwezekanavyo ili kutekeleza mageuzi ambayo tunatambua kuwa yanahitajika kutoa huduma kwa Walebanon.” Amesema Macron 

 Macron alikuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kuitembelea Lebanon, baada ya mlipuko wa Beirut uliowauwa watu 188 na kuwajeruhi maelfu ya wengine. Aliahidi kurejea Septemba mosi kushiriki katika matukio ya kuadhinimisha miaka 100 ya uhuru wa Lebanon kutoka kwa Ufaransa.

Magufuli aanza rasmi Kampeni
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 1, 2020