Madaktari Bingwa Wa Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Dodoma wameweka kambi na kuanza upasuaji kwa wagonjwa wenye uhitaji wa huduma hiyo, katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete.

Kiongozi wa madakatri hao, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Pwani – Tumbi, Dkt. Amani Malima amesema kazi hiyo itadumu kwa siku tano ambapo wameanza kwa kuwaona na kuwachambua wagonjwa na wenye uhitaji wa upasuaji, wameanza huduma hiyo.

Amesema, “jana tulifanya upasuaji kwa watoto wenye matatizo ya masikio, koo na pua pamoja na matumbo, kwa hiyo leo tunaendelea kwa upande wa idara ya mifupa hususani kwa watoto wenye matatizo ya mifupa ambayo wamezaliwa nayo.

Aidha, Dkt. Malima ameongeza kuwa lengo la kambi hiyo ni kutoa huduma za matibabu ya kibingwa wa wananchi wa mkoa wa Tabora, na kuwapunguzia gharama za kuzifuata huduma hizo nje ya mkoa ikiwemo kwenda Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza na Kilimanjaro.

“tumeona ni vyema kujiongeza licha ya kuwapunguzia gharama Watanzania wa kuzifuata huduma hizi nje ya Tabora, tutawajengea uwezo wataalamu wa hospitali hii, ili wananchi waendelee kupata huduma, tumeunda kikundi cha madaktari bingwa kutoka fani mbalimbali zaidi ya 20.” amesema.

Zanzibar kupima ubora wa Bidhaa kwa viwango vya Kimataifa
Kimbunga Freddy: Rais atangaza wiki mbili za maombolezo