DRC, Madaktari nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaendelea na mgomo wao walioanza siku ya Jumatatu Aprili 23 mwaka huu.

Madaktari nchini DR Congo wanaomba Serikali kuboresha mishahara yao, huku wakiishutumu kutoheshimu makubaliano walioafikiana mwaka jana kuhusu madai yao.

Madaktari wanataka kupewa mshahara mzuri, malipo ya kazi zao za ziada, kutambuliwa kwa vyeo vyao na ufumbuzi kwa madaktari mia moja waliyofukuzwa kinyume cha sheria mwaka 2016 kwa mujibu wa madaktari hao, na ambao hufanya kazi tangu wakati huo bila malipo.

Pia wanalalamikia makubaliano ya hivi karibuni yaliyosainiwa Septemba 2017 na yangelipaswa kutatua masuala yote hayo yanayozua utata, ambapo wameeleza kuwa makubaliano hayo hayajawahi kutekelezwa.

Aidha, wagonjwa wameomba madaktari kusitisha mgomo huo wakisema kuwa unawaathiri pakubwa, huku wakiomba Serikali kutafutia ufumbuzi madai ya madaktari.

Serikali ilitoa mapendekezo kwa madaktari wanaogoma huku ikieleza kwamba tayari imejibu madai ya madaktari, ambapo kazi kubwa kwa sasa iko upande wa chama kikuu cha madaktari, ambacho hakikuwasilisha mapendekzo hayo kwa wanachama wake.

Awali, Madaktari humo walitangaza kuwa watafanya mgomo wa nchi nzima siku ya Jumatatu ijayo Aprili 23 mwaka huu kufuatia madai yao kushindwa kutekelezwa na Serikali.

Jopo la madaktari limetoa tangazo Alhamisi wiki hii kuwa hatua zote zimefuatwa, na kwamba Waziri Mkuu wa nchi hiyo Bruno Tshibala amepewa barua yenye mapendekezo yaliyokubaliwa na pande zote mbili, lakini hakuna majibu yoyote ametoa.

Waziri Ummy azindua ugawaji wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu Kigoma
Mkuu wa majeshi afutwa kazi